Serikali Mkoa wa Singida imewakaribisha wadau mbalimbali kuja kuwekeza kwa kuanzisha Viwanda vikubwa,vya kati na vidogo kutokana na mkoa huo kuwa na umeme mwingi unaobaki baada ya matumizi
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Muragiri pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kwakuwakaribisha wadau mbalimbali kuja kuwekeza mkoani hapa kwani nishati ya umeme ni ya uhakika
Wataalamu wetu wametuambia mkoa wetu unapokea umeme wa megawatt 232 wakati matumizi halisi ni megawatt 10,hivyo kuna umeme mwingi unaobaki..waje wajenge viwanda." alisema Muragiri
Aidha kwa upande wa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Ilani amewahakikishia wajumbe kuzitatua changamoto hizo kwa kuwaagiza Viongozi wa sekta na Idara mbalimbali za Manispaa kwenda kusimamia ipavyo huku wakitafuta njia za kumaliza changamoto chache zizojitokeza
Zipo changamoto kama upungufu wa WOD za wazazi katika kituo cha afya Sokoine kutokana na kituo hicho kupokea zaidi ya wanawake 800 kwa mwezi wanaokwenda kujifungua, Serikali imejipanga kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wetu na kukipandisha hadhi kituo hicho na kuwa Hospitali ya Wilaya jambo litakalo saidia kuondoa changamoto za upungufu wa WOD." alisema Muragiri
Baada ya wajumbe hao kuipokea taarifa hiyo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya Lucia Mwiru aliwataka wakuu wa Idara kuhakikisha zile kasoro chache zizojitokeza zinatatuliwa mapema kwa maslahi ya wananchi ili pia wananchi waendelee kukiamini chama hicho
Na Ismail Luhamb,Boniphace Jilili, Singida
0 Comments