Recent-Post

Rage: Manara yuko sahihi


 Muacheni  Haji Manara atafute maisha! hiyo ni kauli ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismail Rage baada ya msemaji huyo kuhamia kwa watani zake Yanga.

Manara jana alikuwa habari ya mjini baada ya kutangazwa kuwa Msemaji mpya wa klabu ya Yanga baada ya iliyokuwa klabu yake ya Simba kuachana nae akituhumiwa kuhujumu timu hiyo.

Soma zaidi: Mbunifu jezi mpya Yanga afunguka

Akizungumza na Mwanaspoti Online Rage amesema kuondoka kwa Manara Simba kwenda Yanga ni kutafuta riziki hivyo wasimbeze kwa kuwa ni katika kupigana na maisha.

Rage amesema Manara hajaenda Yanga kama mwanachama bali ameenda kufanya kazi kama ile aliyokuwa akiifanya Simba.

"Mimi namtakia mafanikio mema huko alikoamua kwenda, kwani alichokuwa akikifanya Simba ndio kile kile anaenda kukifanya akiwa Yanga, hivyo tumpe mkono wa kheri tu akafanikiwe,"anasema Rage.

Aidha Rage anasema, mbali ya kuondoka ameacha alama kubwa ndani ya Simba ambayo haitaweza kufutika kutokana na mchango wake mkubwa wa namna ambavyo aliibrand timu hiyo.

"Kwanza kabisa jana alikuwa smart sana katika utambulisho wake, hakutaka maswali ndio alikuwa sahihi kabisa najua swali la kwanza lingeuliza juu ya uanachama wake na alijua hilo akakwepa ni sawa kabisa,"

Post a Comment

0 Comments