TANO BORA YA UTUPIAJI, SIMBA WATAWALA

KATIKA safu kali ya ushambuliaji kwa msimu wa 2020/21 namba moja ilikuwa ni ile inayotoka kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kilichotwaa ubingwa kikiwa na pointi 83.

Rekodi zinaonyesha kuwa mbali ya kuwa ni namba moja katika utupiaji  na kwenye chati ya ufungaji bora ndani ya tano bora washambuliaji kutoka Simba walitawala eneo namna wanavyotaka.

Ndio walifanya hivyo na hiyo iwape hasira wale ambao wamepanda Ligi Kuu Bara msimu huu ambao ni Geita Gold pamoja na Mbeya Kwanza kupambana kwa hali na mali kuyapata mafanikio. 

Katika tano bora ya utupiaji ni wachezaji wawili pekee hawakuwa mali ya Simba hivyo wangezubaa kidogo pennine orodha kuanzia namba moja mpaka ile ya tano ingekuwa mikononi mwa Simba.

Ni Idd Seleman wengi wanapenda kumuita Nado huyu ni mali ya Azam FC alitupia mabao 10 wakati timu yake ya Azam FC ulitupia jumla ya mabao 50 katika michezo 34 na ilimaliza nafasi ya tatu na pointi 68.

Nado alitupia mabao 10 na kuwa ndani ya tano bora sawa na staa kutoka JKT Tanzania,  Danny Lyanga ambaye naye alitupia mabao 10 katika mabao 34 yaliyofungwa na timu yake ambayo ilimaliza ikiwa nafasi ya 15 na pointi 39 lakini msimu wa 2021/22 itashiriki Ligi Daraja la Kwanza na kwa sasa inaitwa Championship.

Mwingine ni Prince Dube huyu ni namba tatu kwenye orodha ni kutoka Azam FC pia huyu aliuwasha moto kwelikweli ila majeraha ya nyama za paja pamona na maumivu ya tumbo yalizima kasi yake na kumfanya amalize akiwa na mabao 14.

Utatu kutoka Simba ulikuwa unaongozwa na nahodha mzawa ambaye ni wa kwanza kufunga mabao zaidi ya 100 kwenye ligi, si mwingine ni John Bocco alitupia mabao 16 alikuwa namba moja.

Namba mbili alikuwa ni Chris Mugalu alitupia mabao 15 ikumbukwe kwamba ulikuwa ni msimu wake wa kwanza na ile ya nne ilikuwa mikononi mwa Meddie Kagere aliyetupia mabao 13 na alikuwa ni mfungaji bora mara mbili mfululizo kuanzia msimu wa 2018/19 alipotupia mabao 23 na 2020/21 alipotupia mabao 22.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments