Gwajima adai mahubiri ndiyo yalimponza

Siku tano baada Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kupewa adhabu na Bunge ya kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge akilipwa nusu mshahara, ameeleza ilivyokuwa akidai mahubiri yake ndiyo yalimfikisha kwenye Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

Gwajima amesimulia hayo wakati akihubiri katika Kanisa la Ufufuko na Uzima huku akibainisha kuwa mashtaka yaliyomfikisha mbele ya kamati hiyo ni mahubiri aliyotoa madhabahuni.

Soma hapa: Askofu Gwajima ahojiwa akiwa amesimama Kamati ya Bunge

Akizungumza katika ibada hiyo leo Septemba 5, Gwajima amesema aliieleza kamati hiyo kwamba haoni kama wamefanya vizuri kwa sababu yote aliyotuhumiwa nayo aliyahubiri madhabahuni.

“Kama ingetokea nimezungumza kitu nje ya madhabahu hii ni sawa. Niliiambia kamati hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuuliza maswali juu ya imani ya watu na juu ya ibada inayofanywa kanisani,” alisemaAskofu Gwajima huku akishangiliwa na waumini.

Amesema Katiba ya Tanzania inasema Serikali haina dini ila mtu mmoja mmoja ana dini, hivyo wao wana imani yao na hakuna wa kuwabadili.

Post a Comment

0 Comments