KAMWAGA ASEMA KUELEKEA SIMBA DAY KILA KITU FRESH,TP MAZEMBE KUWASILI KESHO

 KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam imesema maandalizi kuelekea Simba Day ambayo ni Septemba 19 mwaka huu yamekamilika na kwamba timu ya TP Mazembe ya nchini Congo DRC inatarajia kuingia kesho kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo.


Wakati kwa upande wa maandalizi ya timu ya Simba iliyokuwa imepiga kambi kwa ajili ya kuajiandaa na msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2021/2022 yamekamilika na kabla ya Arusha timu hiyo ilikuwa imeweka kambi yake nchini Morroco.

Akizungumza leo Septemba 17 ,2021 jijini Dar es Salaam Kaimu Msemaji wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema kuwa kila kitu kiko sawa kuelekea Simba Day na iwapo kutakuwa na changamoto za hapa na pale watazitolea ufafanuzi.

Kamwaga  kuhusu ujio wa TP Mazembe amesema wameonesha heshima kubwa kwa Klabu ya Simba na Tanzania kwa ujumla kwani Chama cha Soka nchini kwao kimeamua kusogeza mbele mchezo wa TP Mazembe ili kuwapa nafasi ya kucheza na Simba katika Simba Day ambayo itakuwa Jumapili ya wiki hii.

 "TP Mazembe watakuja nchini kesho wakitokea Morroco ambako wamepiga kambi, tunajua walikuwa na mchezo mwingine katika nchi yao lakini kwa ukubwa wa Simba na ukubwa wa Simba Day wameamua kuja kuunga nasi kuashimisha siku yetu ambayo ni maalum kitambulisha wachezaji wetu na mashabiki na wapenzi kuiona timu yao ikiwa uwanjani.

"Kwa timu yetu ya Simba tunafahamu baada ya kutoka Morroco ambako tuliweka kambi ,tulienda Arusha kwa ajili ya kuendelea kujianda na msimu mpya wa ligi kuu,mwalimu( Kocha) kwa kushirikiana benchi lake la ufundi wamefanya kazi kubwa kukisuka kikosi chetu, kiko imara na kiko tayari kwq mapambano.Leo kitaondoka Arusha kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya Simba Day,"amesema Kamwaga.

Amesema ni matarajio ya Klabu yao kwamba mashabiki,wanachama na wapenzi wa soka watajitokeza kwa wingi katika Simba Day kwani ni siku ambayo wachezaji watatambulishwa lakini kubwa zaidi wataonesha namna wanavyosakata kabumbu.

"Timu iko vizuri katika kipindi cha maandalizi tumecheza mechi tano za kirafiki,benchi la ufundi limesuka kikosi chake vizuri,wameangalia mifumo ya aina mbalimbali.Na hayo yote tutaanza kuyaona kwa Mkapa siku ya Simba Day.Mwalimu anasema kuna kitu ameongeza kwenye timu yake,hivyo Wana Simba twendeni tukaone hicho kilichoongezwa,"amesema Kamwaga.

Akifafanua kuhusu maandalizi ya Simba Day ,amesema mambo yanakwenda vizuri ingawa kuna changamoto kidogo ilijitokeza kwa upande wa tiketi za N- Card lakini uongozi umefanya mazungumzo na kila kitu kitakuwa sawa.

"Hadi kufikia leo tiketi za Platnum zimemalizika na hata VIP A  zimekwisha, hivyo bado tumebakiza mzunguko na tunawaomba mashabiki waendelee kukata tiketi,"amesema.

Wakati huo huo mashabiki wa Klabu ya Simba wamejihamba kuujaza uwanja wa Mkapa katika Simba Day kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ukubwa wa timu yao,hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Kwa upande  wake mshabiki  K Mziwanda amesema kwa ukubwa wa Simba hawafurahishwi kuona wakifananishwa na vitimu vidogovidogo ,bali wao wanatakiwa kufananishwa na wakubwa wenzao kama Al  Alhal si vinginevyo.

"Sisi hatutaki kupanda mageti ili kuingia uwanjani lakini wao wanataka kujaza uwanja Kwa mashabiki wa Simba kuingia uwanjani Kwa kukata tiketi na kuruka mageti,"amesema na kuongeza kwa ukubwa wa Simba unaonekana hadharani na kuna uwezekano wa kujaza na kiwanja cha Uhuru ' Shamba la bibi' kutokana na wingi wa wana Simba.

                                                                   Na Said Mwishehe

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments