Kina Sakho, Mayele waipa kicheko TRA

 

ONGEZEKO la nyota wa kigeni kutoka 10 hadi 12 imeipa kicheko Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwani imewaongezea mapato zaidi wanayokata kwa wageni katika kukusanya kodi michezoni.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema uwepo wa wachezaji wa kigeni katika klabu za soka unainufaisha nchi kwa kodi wanazowakata.

Kayombo alisema hata nyota wa kigeni katioka soka wanakatwa kodi ya kulingana na mapato chake(PAYE) kama wachezaji wa ndani au wafanyakazi wengine wa kawaida, hivyo wanavyokuwepo ni neema kwa nchi kwenye mapato.

“Mishahara ni mapato wanayopata ndani ya nchi na sheria inatambua ukipata pato lolote ndani ya nchi lazima ukatwe kodi,” alisema Kayombo, japo hakuja asilimia ya makato hayo au namna kwa mwaka wanavyovuna kodi hizo, ila alisisitiza wanakatwa kama wanavyokatwa watu wengine.

Klabu za Simba, Yanga na Azam zenye kusajili wageni kila msimu ikiwamo msimu huuu kuwabeba kina Pape Sakho, Fiston Mayele, Idris Mbombo na wengine.

Pia Kayombo alisema faida nyingine inayokuwepo ni kodi zinazotokana na viingilio vya mashabiki kuangalia mpira, mauzo ya jezi na uhamisho wa wachezaji na kukiri changamoto imekuwa kwa klabu ndogo zimekuwa na changamoto kwenye ukusanyaji wa kodi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments