Wananchi wa Algeria wameitaka serikali ya Ufaransa ilipe fidia kwa hasara zilizosababishwa na majaribio yake ya nyuklia iliyofanya ndani ya nchi hiyo katika muongo wa 60 wa karne iliyopita. |
Sambamba na kuwadia kumbukumbu ya majaribio hayo ya nyuklia yaliyofanywa na Ufaransa nchini Algeria, watu wa nchi hiyo wanasema, serikali ya Paris inapasa iombe radhi na kulipa fidia pia kwa hasara za kimaada na kimaanawi walizopata walioathiriwa na tukio hilo.
Wakati huu inaadhimishwa kumbukumbu ya jinai ya nyuklia ya Ufaransa nchini Algeria, jinai ambayo ilitokea katika ardhi ya nchi hiyo baina ya mwaka 1960 hadi 1966
Eneo la ardhi ya Algeria lilipofanyika jaribio la nyuklia la Ufaransa |
Waalgeria laki moja na nusu, ambao baadaye vyombo vya habari viliwaita "panya wa maabara" waliathirika kutokana na mionzi ya nyuklia ya majaribio hayo.
Licha ya hatua ya Ufaransa ya kudhibiti na kuchuja taarifa za maafa hayo, Waalgeria 30,000 walibainika kuwa walipoteza maisha kutokana na majaribio hayo ya nyuklia.
Mafuvu ya Waalgeria 18,000 yamehifadhiwa katika makumbusho moja iliyoko mjini Paris.
0 Comments