ALIYOYASEMA KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO MBELE YA WAJUMBE MKUTANO MKUU MAALUM...AMSHUKURU RAIS SAMIA

 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mainduzi CCM Daniel Chongolo amewahakikishia wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama hicho Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Samia  Suluhu Hassan kwamba kwa kushirikiana na sekratarieti ataendelea kutekeleza majukumu makubwa ya Chama katika nafasi ya utendaji aliyonayo.


Chongolo amesema hayo leo Aprili 1 mwaka huu mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa ambapo amesema leondio mara yake ya kwanza kusimama kwenye Mkutano huo tangu alipoteuliwa Katibu Mkuu.

Kabla ya kuwasilisha maelezo kuhusu Mkutano Mkuu maalum,Chongolo ametumia nafasi hiyo kueleza  leo ndio mara yake ya kwanza kabisa kusimama mbele ya mkutano mkuu wa CCM Taifa akiwa Katibu Mkuu Taifa ,hivyo akaomba kueleza  machache.

"Kwanza kabisa namshuru Mungu kwa kutujaalia neema  yaa uhai na afya njema na leo tunakutana hapa.Naomba kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa kwa uamuzi wenu wa busara mlioufikia kwenye ukumbi huu wa Jakaya Kikwete siku ya Aprili 30 ya mwaka 2021 kwa kumchagua tena wa kura zote mpendewa wetu Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wetu.

"Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wangu na Mwenyekiti wa Chama chetu ndugu Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kupendekeza jina langu mara baada ya kumaliza kwa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ili nichaguliwe kushika nafasi kubwa ya utendaji katika chama chetu

"Aidha kwa mara nyingine tena ninawashukuru wajumbe wote wa Halmashauri Kuu Taifa kwa uamuzi wao wa kukubali kunichagua kuwa Katibu Mkuu, Mimi na wajumbe wenzengu wote wa sekretarieti tutahakikisha tunatekeleza majukumu yetu.

"Kwa hakika Chama hiki kikubwa ambacho sio tu kina wachama ,wapenzi na wakereketwa wengi kushinda chama kingine chochote cha siasa nchini Tanzania bali kinabeba matumaini ya waliyo wengi na kwa ridhaa ya wananchi kitaendelea kuwa dhamana kwa muda mrefu ili kilete maendeleo katika nyanja zote zote za maisha ya binadamu,"amesema Chongolo.

Amesisitiza kuwa kwa kuzingatia ukweli huo amemhakikishi Mwenyekiti wa Chama hicho na Wana CCM wote kuwa hatawaangusha."Ninapenda kuwathibitishia wajumbe wa mkutano mkuu taifa pamoja na wana ccm wote kwa kushirikiana na wezangu nitatekeleza majukumu yangu ya ujenzi wa Chama chetu kwa bidii, nidhamu na weledi mkubwa."

Kuhusu Mkutano Mkuu Maalum  wa Chama hicho,Chongolo amesema kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CCM inaeleza  mkutano mkuu WA CCM Taifa utafanya mikutano mitatu kila baada ya miaka mitano, mikutano miwili kati ya hiyo itakuwa ya uchaguzi na mmoja utakuwa wa kazi.

Ameongeza kalenda ya vikao vya Chama itaeleza ni lini mikutano hiyo inafanyika , lakini mkutano usiokuwa wa kawaida unaweza kufanyika wakati wowote ukiitishwa na Mwenyekiti wa CCM  au ukiombwa na theluthi mbili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa."Taarifa ya kukutana kwa mkutano  huo unatakiwa kutolewa si chini ya miezi miiwili kabla ya tarehe ya kukutana lakini inaweza kutolewa muda mfupi zaidi huo wa kawaida."

Na Said Mwishehe.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments