Mbunge Ataka Wanasaikolojia Waajiriwe Kukabili Mauaji

 Mbunge wa viti maalum (CCM), Ester Maleko ameitaka Serikali kuajiri wataalam wa saikolojia kwa ajili ya kusaidia kupambana na mauaji na ukatili wa kijinsia ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara nchini.

Katika swali lake la nyongeza leo Ijumaa Mei 6,2022, Ester amesema Serikali imekuwa ikifundisha wataalam hao wa saikolojia hadi ngazi ya vyuo vikuu na kuhoji sababu za kutowatumia katika kukabili vitendo hivyo.

Mbunge huyo kutoka CCM pia amehoji sababu za serikali kutounda chama cha wataalam wa saikolojia.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) watashughulikia kupata kibali kwa ajili kuwaajiri wataalam kwa kadri wa bajeti itakavyoruhusu.

Kwa upande wa usajili wa chama, Mwanaidi amesema wako katika mchakato wa kutunga sheria na wataalam wa ustawi wa jamii na utakapomalizika bodi hiyo itaundwa kwa ajili ya kusajili watalaam hao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments