Rais Samia ampa agizo Bashungwa usimamizi fedha za Uviko-19

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Innocent Bashungwa kusimamia zabuni za ununuzi wa vifaa tiba na kazi zingine kupitia fedha za ustawi wa mapambano dhidi ya Uviko-19.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo wilayani Uyui mkoani Tabora wakati akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo, katika ziara yake ya mkoa huo iliyokwenda sambamba na  ufunguzi wa barabara ya Nyahua –Chanya- Uyui-Tabora.

Katika maelezo yake, Rais Samia amesema kuna zabuni za ununuzi wa vifaa vya afya bado zinasuasua kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa,akimtaka Bashungwa kusimamia vyema eneo hilo.

"Mwisho wa matumizi ya fedha za Uviko-19 Juni mwaka huu, na kwamba fedha zote zinahitajika kutumiwa kwa wakati ili kukidhi vigezo vya kupata nyingine zaidi. Waziri ahakikisha memuagiza Waziri Bashungwa Zabuni zinafanyiwa kazi kwa wakati ili kazi hizo zikamilike kwa wakati.

“Ucheleweshaji wa zabuni hizo utasababisha fedha nyingi kutotumika kwa wakati na kusababisha ukiukwaji wa malengo ya fedha hizo,  suala hilo litasababisha  fedha kurudishwa na kukosa fedha nyingine za maendeleo.Nakuagiza waziri wa Tamisemi  kasimamie hili” amesema Rais Samia

Kuhusu matumizi ya fedha kwenye halmashauri Rais Samia  ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia fedha zinazotolewa na Serikali kwa kazi zilizokusudiwa za kutatua kero za wananchi

Rais Samia amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwenye ngazi ya Halmashauri lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi katika sekta ya afya, elimu, maji hivyo zisimamie na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments