YANGA SC YATAWAZWA MABINGWA WA NBC MSIMU WA 2021/2022

KLABU ya Yanga imefanikiwa kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Coastal Union.


Yanga Sc ilikuwa inahitaji pointi tatu ambazo zingeifanya isifikiwe na timu yoyote ile kwa michezo iliyosalia ya kigi kuu ya NBC.

Mabao ya Yanga yamewekwa kimyani na mshambuliaji wao Fiston Kalala Mayele ambaye alipachika mabao mawili na bao lingine likifungwa na Chiko Ushindi.

Mayeke sasa ataendelea kuongoza ufungaji bora akiwa na mabao 16 akifuatia na mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole.

Post a Comment

0 Comments