GEITA GOLD FC YAWEKA HISTORIA NYANKUMBU

 Geita Gold FC rasmi imecheza michezo 30 katika mashindano ya nyumbani bila kufungwa mchezo wowote (Unbeaten) katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita.

Geita Gold FC imefikisha idadi hiyo ya michezo 30 bila kufungwa, katika mchezo wake dhidi ya Ihefu SC ya Mbeya, ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC Premier League) ambapo wamepata ushindi wa bao 1-0, bao hilo lilifungwa na Mshambuliaji wa timu hiyo, Juma Liuzio katika dakika ya 41.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita Mji, Mhe. Zahara Michuzi amesema wanajivunia timu yao kucheza idadi hiyo ya michezo 30 bila kupoteza (Unbetean) katika uwanja huo wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu, huku akisisitiza kuendelea na ujenzi wa uwanja wao mpya (Geita Stadium) eneo la Magogo mjini Geita.

“Geita Gold FC imefikisha ‘Unbeaten’ 30 katika uwanja wa nyumbani, tunashukuru sana, nitahakikisha inabaki hivyo mpaka pale nitakapo ondoka Geita”, amesema Mhe. Zahara Michuzi.

Mhe. Zahara amesema wataendelea kupambana kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano hayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na hata mashindano mengine.

Baada ya ushindi dhidi ya Ihefu SC na kufikisha michezo 30 bila kufungwa kwenye uwanja wa Nyankumbu, Geita Gold FC wamesogea katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara wakiwa na alama 21 katika michezo 14.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments