MBUNGE PAULINE GEKUL AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI BABATI


***********************

Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mhe. Pauline Gekul, ametoa pongezi kwa Serikali ya Awamu wa Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo jimboni hapo.

Mhe. Gekul ametoa pongezi hizo katika Mkutano wa Hadhara wa Rais, Mhe. Samia uliofanyika katika Uwanja wa Kwaraa mjini Babati leo Novemba 23, 2022 ambapo amesema kiasi cha Shilingi bilioni 1.7 unatekeleza mradi ya Vituo vya Afya, huku bilioni 1.5 zikitekeleza ujenzi wa Shule za msingi na sekondari ambapo kwa mwaka 2022 wanafunzi wameingia darasani katika madarasa ambayo yamekamilika kabisa.

Amesema kuwa, takriban Shilingi milioni 10 zimetumika katika ujenzi wa Ofisi ya Machinga Babati Mjini na wamachinga wanaendelea kufanya biashara zao kwa utulivu.

Mhe. Gekul amesema Jimbo hilo pia limenufaika na Mradi wa TASAF katika Mitaa yote kwa kutumia takriban Shilingi milioni 800.

Aidha, Mhe. Gekul amemshukuru Rais Mhe. Samia kwa kuzindua mradi wa barabara za lami wa takriban KM 8 katika Mji wa Babati. Aidha, amemshukuru kwa ahadi yake ya kuongeza KM 5 katika Mji huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments