Kawaida: Tutawatenga wanaounga mkono uvunjifu wa maadili

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mohammed Kawaida ametaka kivuli cha haki za binadamu kisitumike kuathiri maadili ya vijana nchini.

Kauli yake hiyo inatokana na kile alichokibainisha kuwa, limeingia wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili lililofichwa kwenye kivuli cha haki za binadamu.

Kawaida ametoa kauli hiyo Jumatano ya Aprili 26, 2023 katika hotuba yake mbele ya vijana baada ya kutembelea mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) wilayani Arumeru mkoani Arusha.


Kwa mujibu wa Kawaida, katika haki zote za binadamu alizowahi kuzisoma hakuwahi kuona moja inayotaja kile kinachoisitizwa na baadhi ya wanaoshinikiza mmonyoko wa maadili.

"Kuna tatizo kubwa limeingia nchini kwetu kwa kisingizio cha haki za binadamu. Sikufika mbali kwenye haki hizo lakini nimewahi kuzisoma hii sijuiona," amesema.

Mwenyekiti huyo, amesisitiza kuwa hata dini zote zinazoaminiwa nchini hakuna inayokubaliana na tabia zinazoathiri maadili.

"UVCCM tunawakataa na kuwapinga wote na hatuwaungi mkono wenye tabia za upotevu wa nidhamu.

"Ikiwa wewe ni kiongozi ama laa hatukuungi mkono na tukikujua tutakutenga," amesisitiza.


Kuhusu Muungano

Kawaida amesema ni jukumu la vijana kuilinda Tanzania na muungano, akisisitiza mipaka isiwagawe kwani uwepo wake umelenga masuala ya kiutawala.

"Watanzania ni ndugu tusibaguane kwa mipaka wakoloni waliyotuwekea, iliwekwa kwa sababu za kiutawala sio kugawana.

"Ndiyo maana leo Kawaida ni kijana kutokea Unguja Kusini amekubali kuwa Morani kwa sababu sisi sote ni wamoja na yeyote anayetaka kuuharibu umoja wetu lazima tumkatae," amesema.

Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM taifa, Edna Lameck amesema wanaopiga kelele kuhusu mradi wa BBT zinatokana na ukweli kwamba wanatamani kuondoa waliopo ili wapate wao nafasi.


"Kelele za chura hazimzuii Tembo kunywa maji, waacheni wapige kelele nyingi pigeni kazi," amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments