Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji Cha Nyuki Bw. Philemon Kiemi Kutoka Tanzania Tarehe 20 May 2023, alitembelea Chuo Kikuu Cha Johannesburg university business school, South Africa Kwa lengo la Kushirikiana katika tafiti za Masoko katika nchi ya South Africa, Lesotho na Swaziland.
Alikutana na Prof. Marwa na ambaye alikuwa ni Mwenyeji wake na kutembelea maeneo ya Chuo hicho katika vitivo mbalimbali Kwajili Ya Kubadilisha Uzoefu.
Katika Mazungumzo hayo, CEO Philemon Kiemi wa Kijiji Cha Nyuki alisema taasisi yake inatambua Ina Imani kubwa na inathamini saana Elimu na Uzoefu walionao Wahadhiri katika Chuo Kikuu Cha Johannesburg hivyo ni Muhimu katika kutimiza malengo ya Uwekezaji wa kampuni yake hapa South Africa.
Aidha Mwenyeji wake, Prof. Marwa alisema Uongozi wa Chuo Upo tayari kushirikiana na Kampuni hiyo na kuongeza kuwa Katika Ulimwengu huu Biashara zinazofanyika zinahusisha saana tafiti Kwa Vitendo(action Research), teknolojia (Use of appropriate technologies) na Ubora wa Mazao na huduma zinazowafikia walaji(Quality control). Pia amesisitiza kuhusu Umuhimu wa kuwekeza kwenye Elimu ya Biashara Kwa ajili ya Maendeleo ya Kampuni kama (Kijiji Cha Unyuki) Kutoka Singida Tanzania.
Prof. Marwa pia amepongeza hatua za Kampuni ya Kijiji Cha Nyuki katika Kushirikiana na Chuo hicho na kuwa ni ya Kishujaa hasa kipindi hichi ambacho tunasherekea Siku ya Nyuki Duniani.
Na Kwa Pamoja Pande zote mbili zimekubaliana kuanza kazi hii ya Mashirikiano Mapema Iwezekanavyo.
Na Mwindishi Afrika Kusini
0 Comments